Lilian Chonya
2 min readFeb 11, 2022

TAHADHARI:

KAMA UNA MIAKA CHINI YA 18 USISOME KILICHOANDIKWA HAPA

Ni kweli kwamba mwanamke ameumbwa kuwa na aibu na ni kitu ambacho binti pale anapovunja ungo tu anaanzwa kufundishwa. Lakini sasa hizi aibu kuna mahali hazitakiwi yaani inabidi mwanamke uziweke pembeni hasa kama uko kwenye ndoa.

Katika kuzurura kwangu huwa napata nafasi ya kuketi na wanawake tofauti na Mimi hupenda kuwauliza maswali tofauti hasa yanayohusu mambo ya ndoa na familia kwa ujumla ili nami nipate kujifunza.

Nilichogundua wengi ambao nimeweza kuzungumza nao wana mawazo fulani ya jinsi mwanamke anavyopaswa kuwa ndani ya nyumba kitu ambacho sio kibaya lakini wengi wanasahau kuwa ndani ya nyumba huwa kuna kitu kinaitwa Chumbani kwa Mke na Mume.

Kuna baadhi ya wanawake wanawaonea aibu mpaka waume zao wakiwa chumbani wanashindwa kusema kitu anachotaka. Anaweka kimitego mwanaume ukute ameshachoka na mizinguko ya siku nzima anakuwa hakuelewi unaishia kununa,sasa ukishindwa kusema Mumeo atajuaje?

Ngoja sasa nikwambia Mambo ambayo wanawake wengi wanashindwa kuwaambia waume zao.

Nataka Kufanya mapenzi na wewe Leo
Katika wanawake 10 basi ni 2 au 3 tu ndio wanaoweza kuzungumza hivi mbele ya waume zao. Wengi wanafikiri wataonekana ni wahuni au malaya, lakini sio kweli kwasababu huyo ni mumeo na moja ya jukumu lake ndani ya ndoa yenu ni kukuridhisha kinwili sasa ukishindwa kusema na kutegemea mpaka aanze yeye kama umezidiwa na hamu yeye atajuaje?Unajua mwanaume ni kiumbe ambaye hapendi kupindisha kona nyingi kama anataka mchezo atakwambia tu basi na wewe nwambie ni mume wako.

  • Leo hujanifikisha kileleni hili nalo huwa ni tatizo wengi hapa hawaongei kabisa eti wanaogopa kuwaudhi waume zao. Wewe unajua kuna wakati vikizidi ndio unakutana na mtu ana visirani havishikiki. Ni haki yako kufika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
  • Huwa nafurahi ukinishika hivi au vile au hapa na pale wakati wa tendo.

Ukiwa ndani ya chumba chako na mume wako aibu zako ziache mlangoni na uzifungie nje humo ndani ni kufurahishana nafsi na kama unashindwa kumwambia kwa mdomo mtumie meseji. Na kuongea na mume wako kuhusu mambo haya sio umalaya au uhuni, inatakiwa iwe kitu cha kawaida baina yenu unafikiri kwanini nyumba ndogo haziishi kwasababu wengi wao wanafahamu kuna sheria za subuleni na sheria za chumbani na ukiwa mbele ya mwanaume aibu na haya zako zifungie kabatini furahia maisha.

Lilian Chonya
Lilian Chonya

Written by Lilian Chonya

Karibu usome nakala zangu kuhusu| Mahusiano | Malezi | Ndoa

No responses yet