Mfanye Mpenzi Wako Atabasamu Kwa Kumtumia Meseji Hizi

Lilian Chonya
4 min readMar 17, 2022

Ulishawahi kushika simu yako ukiwa na lengo la kumtumia mpenzi wako meseji lakini hujui uandike kitu gani unaishia tu kuandika “Vipi umeshakula?”yaani hapo hata Wewe mwenyewe lazima ujione sio, na yeye kule akiisoma ataishia kuzingusha macho juu na kusema huyu nae maswali gani sasa haya yaani amekosa maneno ya kuandika? Upo hapo?

Naelewa hakuna mtu ambae hapendi kumwandikia mpenzi wake meseji nzuri ya kuvutia, lakini shida inakuja mara nyingi hujui uanzie wapi au useme nini na wakati huo huo unataka uonekane wa kiutofauti kwa mpenzi wako. Inakera hiyo kitu acha tu. Unataka kutuma meseji ili mchat kidogo lakini ukifikiria nitamchokozaje ili aweze kujibu unaishia kuweka simu chini au kuingia twitter kuangalia leo vayolensi iko mtaa upi au uingie Instagram uangalie habari mpya. Hizo nyakati mwisho ni leo hii usomapo hapa.

Sasa leo nataka nikwambie umefikia mwisho wa tatizo lako, hapo chini nimekuorodheshea meseji 25 ambazo ukimtumia mpenzi wako lazima huko aliko afurahi na tabasamu juu na hata kama alikuwa hapendi kuchat na Wewe utashangaa jinsi atakavyokuwa na moto wa kupenda na kuendelea kuchat na Wewe kila siku.

1. Wewe ndiye mwenye ufunguo wa moyo wangu nakupenda sana.

2. Kila napokuwa naangalia macho yako mazuri huwa najiona Mimi ni mtu mwenye bahati sana kuwa nawe.

3. Wewe ni mrembo, mtulivu, mpole, myenyekevu na mwaminifu. Hakika nimependelewa na Mungu kuwa na Wewe maishani mwangu. Nakupenda sana.

4.Upendo wako umeleta furaha maishani mwangu na ndani ya moyo wangu.

5. Umeifanya dunia yangu kuwa mahali pa furaha kwa sababu uko ndani yake. Umeigusa nafsi yangu kwa njia ambazo maneno hayawezi kuelezea.

6. Toka siku ya kwanza nilipokuona nilivutiwa na wewe, tabasamu lako, uzuri wako, akili yako. Moyo wangu, roho yangu, na mwili wangu vyote ni vyako Mimi ni wako kabisa Nakupenda sana.

7.Kukupenda ni jambo rahisi zaidi ambalo nimewahi kufanya katika maisha yangu na ni jambo ambalo ningependa kuendelea kulifanya maisha yangu yote.

8.Muda/Miaka ambayo tumekuwa sote imebadilisha mambo mengi sana, lakini jambo ambalo halijabadikika ni jinsi ninavyojisikia kila ninapokuwa karibu na wewe ni huwa najiona ni kama ndio kwanza tunaanza uhusiano wetu.

9.Moyo wangu najua uko salama mikononi mwako mpenzi wangu.

10.Baada ya miaka hii yote ya kuwa pamoja nataka ufahamu kuwa bado unawasha moto ndani yangu ambao ni wewe tu unayeweza kuuzima.

10.Sijawahi kujuta hata dakika moja ya kuwa na wewe katika maisha yangu.

11. Wewe ni kipenzi cha moyo wangu na nuru ya maisha yangu. Wewe ni wa thamani zaidi kwangu kuliko kitu chochote au mtu mwingine yeyote, na nitakuthamini milele.
12. Kila siku ninapoamka na kukuona wewe pembeni yangu huwa najihisi kama nipo ndotoni , ndoto nzuri ambayo kamwe sitaki kuamka kutoka katika huo usingizi. I love you
13. Umenipa kitu muhimu sana ambacho pesa haiwezi kununua, Upendo usio na kipimo.

14. Nazidi kukupenda zaidi kila siku inayoitwa leo na nionapo tabasamu lako ndio unanimaliza kabisa.

15. Umefanya maisha yangu kuwa ya thamani zaidi kuliko nilivyowahi kufikiri hapo mwanzo. Umeniongezea vitu vingi maishani mwangu.

16.Upendo wako umekuwa ndio msukumo wangu wa ndani, motisha yangu, na chanzo cha faraja yangu. Kadiri Navyoendelea kuwa na wewe pembeni yangu, ninajihisi kuwa naweza kufanya chochote, sina hofu tena kwa sababu najua ninao upendo na msaada wako siku zote. Nakupenda

17. Kila unapokuwa mbali na Mimi huwa siwezi kuacha kukufikiria na kutamani urudi ili nikishike tena mikononi mwangu .

18. Umeleta nuru katika maisha yangu na kila siku unanipa nguvu ya kusonga mbele zaidi, asante sana kwa upendo wako kwangu.

19. Umenisaidia kuwa mwanaume/baba bora kwa kila sekunde ambayo umekuwa pembeni yangu. Hakuna mtu ambaye anaweza kunielewa kwa jinsi unavyonielewa wewe.

20. Dunia imekuwa mahali pazuri zaidi kwa sababu wewe upo. Mpenzi wangu wewe ni wa kipekee sana. Natamani ujione kupitia haya macho yangu ya upendo. Mapungufu yako sio kitu na yasikuzuie kutimiza ndoto zako.

21. Upendo wako ndio kitu muhimu na cha thamani zaidi katika maisha yangu, siwezi kukuchukulia kikawaida au kuja kusahau jinsi nilivyo na bahati ya kuwa ya na wewe.

22. Sasa hivi siweza kufikiria maisha yangu bila wewe, ninafuraha sana kwa kuamua kunipa moyo wako, na wewe unao moyo wangu sasa na hata milele.

23.Wewe ni malkia wangu na wa moyo wangu.

24. Tangu siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ya kuwa wewe ndiye mwanamke unayenifaa, upendo nilionao juu yako ni mkubwa zaidi ya uwezavyo kufikiria.

25. Malkia wangu wa nguvu uzuri wako, akili yako, hekima zako sio rahisi kuelezea kwa maneno.

Mapenzi ni vionjo, huitaji kuwa romantiki unachohitaji ni mpenzi wako akuone kuwa unamjali pamoja na meseji nzuri kama hizi ambazo zitaongeza vionjo na utamu kwenye mahusiano yenu. Achana na zile meseji za umekula au unarudi saa ngapi anza kumtumia mpenzi wako meseji hizi, hata kama amekununia kwa wiki nzima ukimtumia makombora ya hizi meseji utayeyusha kabisa hasira zilizokuwa ndani yake juu yako.

Kazi kwako.

--

--

Lilian Chonya

Karibu usome nakala zangu kuhusu| Mahusiano | Malezi | Ndoa