Kama Anavyo Hivi Vigezo 21 Huyo Anafaa Kukuoa

Lilian Chonya
2 min readMar 16, 2022

--

Tupo katika kipindi ambacho wasichana wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa, kiasi cha kwamba baadhi ya wanaume wanachukilia hiyo kama fursa ya kutembea na wasichana tofauti wakiwa ahidi ndoa na mwisho wa siku wanawatafutia sababu wanawaacha. Wanawake wengi wanabaki na vidonda moyoni na wengine huwa wanafikia hatua ya kufanya vitu vya ajabu kutokana na kuumizwa.

Sasa kama na Wewe ni mmoja wa msichana ambaye unatafuta mwanaume wa kuja kufunga nae ndoa na kuanza familia pamoja leo nimekuandalia listi hii ya vigezo au ishara ambayo itakusaidia kufahamu kama uko na mwanaume sahihi.

Mwanaume yeyote ambaye anajielewa na yuko siriasi na Wewe lazima utaziona hizi tabia 21 kutoka kwake:

1. Hatojaribu kukubadilisha ili uwe jinsi anavyotaka yeye
2. Uko huru kuzungumza nae kuhusu kitu chochote bila kufikiria atakuonaje
3. Unapofikiria kuolewa nae, haufikirii sana kuhusu sherehe ya harusi bali ule muda ambao mtaanza kuishi pamoja
4. Anajitoa sana kwa ajili yako na Wewe pia unajisikia fahari na furaha kufanya hivyo pia kwa ajili yake.

5. Unaweza kulia mbele yake bila kujisikia vibaya au kuona aibu.

6. Akikwambia “Nimekumis” unajua hajasema tu bali ana maanisha kweli na hapa siongelei kufanya mapenzi🙄
7. Uko huru kupanga au kumwambia mipango yako.

8. Anakwambia mipango yake na anasikiliza ushauri unaompatia.
9. Haruhusu mtu au watu wakuvunjie heshima uwepo au usiwepo.
10. Mnaweza kuwa mbali lakini mapenzi yenu hayapungui.

11. Yupo karibu na familia yako hata kama hasaidii kifedha lakini anahakikisha kama kuna tatizo atajitahidi aweze kuitatua.

12. Ukiwa na stress zako ukija kwako anakusikiliza uongee mpaka yaishe moyoni mwako.

13. Anaheshimu mipaka yako, anakujali na kukuthamini.

14. Anakuamini na Wewe unamuamini.

15. Anakusifia mbele za watu.

16. Anapenda kuona ukiendelea mbele, atakusapoti, kiakili, kiroho hata kifedha kama anayo.
17. Anakusifia ukipendeza na anapenda kukuona unapendeza.

18. Mnafanya vitu pamoja na hakuna kati yenu anaye boreka.

19. Hata mnapopishana kauli yuko tayari myamalize kabla hamjalala ili kesho muamke mkiwa na furaha.

20. Mnaweza kukaa wawili tu mahali na kila mtu kati yenu akafurahi.

21. Anapofanya kosa anakiri na kuomba msamaha.

Hizi ni baadhi ya tu ya vigezo vya mwanaume ambaye unafaa kuolewa naye. Ila sasa na wewe unapoangalia vigezo hivi hakikisha na Wewe una tabia ambazo zitamfanya hata yeye aseme kuwa hapa nimepata mke.

--

--

Lilian Chonya
Lilian Chonya

Written by Lilian Chonya

Karibu usome nakala zangu kuhusu| Mahusiano | Malezi | Ndoa

No responses yet