Lilian Chonya
2 min readFeb 5, 2022

Jinsi Katuni Hizi 22 Zilivyo Wasaidia Watoto Wangu Kujifunza Vitu Vingi Ndani Ya Muda Mfupi Namba 10 Na 16 Ndiyo Bora Zaidi.

Hivi kuna mtoto ambae hapendi katuni? Mzazi unaweza usizipendena usitake kabisa wanao waziangalie lakini kwa mtoto huwa ni kitu tofauti. Mtoto anaweza akaketi hata masaa matatu anaitazama katuni hiyo hiyo bila kuchoka.

Hata Wewe wakati wa utoto wako nafahamu uliangalia sana katuni za wakati ule zile za Tom& Jerry, John Bravo, The Powerful Girls, Cow& Chicken na nyingine nyingi na nina uhakika kuna vitu ambavyo ulijifunza kupitia hizo katuni na bado unavikumbuka hata sasa unaposoma hapa.

Siku hizi maneno yamekuwa mengi sana mtaani kuhusu katuni, sawa baadhi ya maneno hayo yasemwayo ni kweli lakini unafahamu kwamba kuna katuni ambazo mwanao akiwa anazitazama zitamsaidia kujifunza na kuelewa vitu vingi ambavyo hata wewe inawezekana huvijui au akikuuliza itakubidi uingie kwanza google kutafuta majibu?

Mwaka 2020 wakati Covid ilipoanza na watoto wakatakiwa kukaa nyumbani, ilinibidi kukaa chini na kutafakari ni vipi nitawasaidia wanangu waendelee kujifunza wakati wakiwa nyumbani? Sina mwongozo wala sifahamu chochote kuhusu kufundisha ila hamu yangu ilikuwa ni kuwaona wakiendelea kujifunza.

Hapo ndipo nilipoingia YouTube na kuanza kutafuta Video za kujifunza kwa watoto. Nilianza kwa kuandika (learning video for 5 year old)zikaja hapo nikachagua zile ambazo nilihisi zinafaa nikazitizama kwanza mwenyewe ili nijihakikishe zina maudhui ninayotaka kisha nikazi download na kutafuta za mtoto wa miaka 2 na zenyewe nikazi download kisha nikaweka kwenye flash drive ili wawe wanaziangalia kutokea kwenye TV.

Ninachoweza kusema ni kwamba baada ya muda mfupi tu toka kuanza kuangalia zile katuni sio wao waliokuwa wanajifunza hata Mimi pia nilijifunza na mpaka kuna siku nikawaza hivi mbona Sisi hatukufundishwa hivi ningekuwa genius mimi 😅

Kwakuwa wanasema kizuri kula na nduguyo hapa chini nimekuwekea katuni zote ambazo watoto wangu zimewasaidia sana na zinafaa kuangaliwa na mtoto wa miezi 3 na kuendelea. Mtoto wa miezi 3 anaweza kuangalia kwasababu mtoto anaweza kuona rangi na zile rangi rangi za kwenye katuni zitamsaidia kuusisimua ubongo wake lakini hakikisha unapunguza mwanga wa simu au TV ili kuepuka kumuumiza macho mtoto.

  1. Na hii ndio list ya hizo katuni ukiingia YouTube zitafute zina maudhui bora hilo nimethibitisha
    1. Dave& Ava.
  2. Cocomelon.
  3. Baby Tv.
  4. Jojo English.
  5. Farmees.
  6. Little Baby Bum.
  7. Chuchu Tv.
  8. Rock & Learn.
  9. Kids Diana show.
  10. Preschool Prep company (hii ni ya hesabu)
  11. Genevieve’s play house.
  12. Bob the train.
  13. T- series kids tv.
  14. Peekabookidz.
  15. Vlad & Niki
  16. Alphablocks
  17. Monica J Sutton.
  18. Learning time fun.
  19. Kiddos world tv.
  20. Blippi.
  21. Tutitu tv.
  22. Busy Beavers

Ni matumaini yangu baadae utakapompatia mwanao simu ili aangalie katuni huku wewe ukiwa unaendelea na shughuli zako, utamtafutia moja kati ya hizo channel ili aiishie tu kuangali bali na kujifunza pia.

Lilian Chonya
Lilian Chonya

Written by Lilian Chonya

Karibu usome nakala zangu kuhusu| Mahusiano | Malezi | Ndoa

No responses yet