Instagram ni mtandao ambao ni rahisi sana kuutumia. Unaweza kusema kwakuwa Wewe umeshaujulia ndio maana unasema hivyo, ni kweli lakini si ndio sababu nikaamua kuandika nakala hii ili na Wewe uweze kujifunza kupitia haya ambayo naandika hapa.
Baada ya kuanza kuutumia mtandao wa Instagram kibiashara toka mwaka 2019 kuna vitu ambavyo nimejifunza na ambavyo vilinisaidia sio tu kukuza akaunti kufikia watu elfu 13.3 bali hata kupata dili za kutangaza biashara za watu na kuzikuza akaunti nyingine tofauti.
Kuna mambo 10 ya muhimu ambayo lazima uyazingatie ili uweze kukuza akaunti yako ya Instagram ambayo ni :
1. Jinsi ulivyo iandika Bio yako
Hii ndio utambulisho wako, mtu ataiona post yako kwenye sehemu ya search akivutiwa nayo atakuja kwenye profile yako na atakacho angalia kwanza ni Bio, Wewe ni nani na unafanya nini. Hivyo basi zingatia jinsi unavyoiandika Bio yako ili impatie mteja mtarajiwa majibu ya haraka ya maswali yake kama: huyu ni nani, anafanya nini, yuko wapi, muda wake wa kazi ni upi na nitampataje kwa urahisi nikihitaji huduma yake.
2. Muda Sahihi wa kupost
Kama biashara yako ina walenga Watanzania basi muda sahihi wa kuposti ni
- Saa tatu asubuhi,
- Saa sita mchana,
- Saa tisa mchana,
- Saa kumi na mbili jioni
- Saa tatu usiku. Hii ndio mida ambayo watu wengi wanakuwa online. Chagua muda ambao utaona unakufaa kati ya hiyo hapo juu na upost.
3. Post Mara 3 au 4 kwa siku
Hizi unaweza ziona ni post nyingi hasa kama ukiwa hujui upost kitu gani lakini kwa jinsi unavyoendelea post ndivyo algorithm ya Instagram itakavyo zichukua post zako na kuziweka kwenye ile sehemu ya search bar ili zionekane na watu wengi zaidi. Kwa hiyo kwa jinsi unavyozidi kupost unajiongezea nafasi ya post zako kuonekana kwa watu wengi.
4. Tumia Hashtags
Zamani Instagram ilikuwa tunatumia hashtags mpaka 30, lakini siku hizi mambo yamebadilika ili Instagram iweze kutambua akaunti yako inajihusisha na nini na iweze kukusaidia kuonyesha post zako kwa watu sahihi wanashauri utumie hashtags zisizozidi 8 na ziwe zinaendana na kile unachokifanya. Hizi hashtags usizibadilishe zitumie hizo hizo katika kila post lakini ziweke ile sehemu ya comment.
5. Andika caption
Usiweke tu picha na kuiacha kama ilivyo,mteja wako hatofahamu ujumbe uliokusudia, jitahidi uielezee hata kwa maneno mawili matatu. Na kama unashindwa kuandika kabisa caption ingia google na tafuta caption for…kutegemeana kile unachokifanya. Ukizipata jaribu kuzibadilisha kuja kwenye kiswahili kwa kutumia google hiyo hiyo🤭.
6. Post picha nzuri
Hapa ndipo mtihani kwa wengi lakini, kwenye Instagram picha nzuri ndizo zinazovutia zaidi na Instagram wenyewe wanazipenda. Kama huna picha usihofu ingia kwenye app ya Pinterest na tafuta picha kisha download na zitumie au unaweza kuzitafuta google free videos/images itakuletea websites ambazo zina picha nyingi tofauti.
7. Jibu comments na DM
Hizi ni muhimu kwani unatengeneza mahusiano na wateja wako na hata ikitokea mtu ameandika vibaya wewe mjibu vizuri kwani hiyo ni biashara yako na uko hapo kupata wateja.
8. Usiweke ukurasa wako Private
Ukiwa mfanyabiashara epuka kuweka ukurasa wako private ni muhimu sana uwe public kwani kuna watu ambao wanaitumia mitandao lakini hawapendi mambo ya kufollow anataka akiona bidhaa na ameipenda anakutafuta mnamalizana.
9. Usifanye mchezo wa ku follow na unfollow au kuwa follow mastaa na kuwa unfollow ili upate followers.
Kama unataka watu sahihi kwa ajili ya bidhaa zako basi ni bora ukaikuza akaunti yako kikawaida kwa kufuata hizo hatua nilizo kuandikia hapo juu. Kufanya michezo ya follow na unfollow mara zote itakuletea watu tofauti na unao walenga wewe.
10. Jipe muda walau siku 90
Kitu ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa ukiwa na nia ya dhati ya kuikuza akaunti yako na kujikusanyia watu watakaopendezwa na kufuata hicho unachokifanya badi akaunti yako itakua, Wewe jipe siku 90 ambazo utazigawa katika siku thelathini thelathini na ili uweze kuyaona matokeo.
La mwisho kabisa chonde chonde usinunue akaunti ya mtu, hufahamu huyu mtu alikuwa na watu wa aina gani ambao walikuwa wamezoea kuona maudhui gani, Wewe kuza akaunti yako kwa urahisi tu kwa kufuata hizi hatua.
Kama una maswali usisite kuniuliza nitakujibu.